Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ameagiza kusitishwa mkataba wa mkandarasi kutoka China, Shandong Luquiao Group, anayejenga barabara ya Omurushaka –Kyerwa yenye urefu wa kilometa 50 iliyopo mkoani Kagera kwa kusuasua katika utekelezaji licha ya kulipwa zaidi ya Shilingi Bilioni tisa.
Ulega amesema sheria zitafuatwa, mkandarasi huyo asipewe kazi tena nchini, na wanaosababisha hasara kwa serikali ikiwemo uzembe wa kisheria wachukuliwe hatua.
Ameelekeza TANROADS kuvunja mkataba ndani ya mwezi mmoja na kumpata mkandarasi wa ndani mwenye uwezo ili kuharakisha ujenzi wa barabara hiyo ya lami.
Mhariri @moseskwindi
(Feed generated with FetchRSS)