‎#HABARI: Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imewataka wadau na wafanyabiashara kutoka taasisi mbalimbali kuweka kipaumbele katika kukuza na kutangaza bidhaa zinazotengenezwa nchini, ili kuimarisha uchumi na kuinua viwanda vya ndani.

‎Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba), Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Latifa Khamis, amesema ni muhimu kwa Watanzania kuunga mkono bidhaa za ndani ili kuongeza ajira, mapato na ushindani wa bidhaa za Tanzania katika soko la kimataifa..

‎Maonesho hayo ya SabaSaba mwaka huu yanatarajiwa kuvutia washiriki wa ndani na nje ya nchi, yakiwa na dhamira ya kuhamasisha matumizi ya bidhaa za kitanzania na kukuza ushirikiano wa kibiashara.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *