Maafisa ununuzi na ugavi 120 kutoka kanda zote za Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), wanashiriki mafunzo elekez…Maafisa ununuzi na ugavi 120 kutoka kanda zote za Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), wanashiriki mafunzo elekez…

Maafisa ununuzi na ugavi 120 kutoka kanda zote za Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), wanashiriki mafunzo elekezi jijini Dodoma ili kuwajengea uwezo katika kazi zao.

Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi, VETA, Witness Mgimba amesema mafunzo hayo yameanza Machi 6 hadi 12, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha VETA Dodoma kwa kushirikiana na maafisa ununuzi wa VETA makao makuu, wataalam kutoka PPRA na wataalam kutoka Hazina.

“Mafunzo haya yanalenga kuimarisha utendaji kazi, kuhakikisha ufanisi, utunzaji wa mali za umma, matumizi ya mfumo wa Uhasibu Seriakalini (MUSE), kushirikisha makundi maalum katika ununuzi wa umma na kufuata taratibu za Serikali katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku,” amesema Mgimba.

Kwa upande wake Jacqline Sebastian, Afisa Ununuzi Mwandazi kutoka MVTTC amesema amejifunza kuhusisha makundi maalum kwenye ununuzi wa umma yanayojumuisha wanawake, vijana, wazee na watu wenye ulemavu.

Paul Mshabaha, Afisa Ununuzi kutoka Chuo cha VETA Iringa na mnufaika wa mafunzo hayo ameishukuru VETA kwa kuandaa mafunzo haya hasa kwa ajira mpya kwani inasaidia utunzaji wa mali za serikali,mfumo wa ulipaji Serikalini (MUSE), lakini tunatarajia kujifunza maadili ya utumishi umma.

VETA imekuwa ikitoa mafunzo elekezi kwa watumishi wa kada ya ununuzi na ugavi ili kuelewa majukumu na kuwajenga uwezo ili kufikia malengo ya Serikali na kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa ufanisi.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *