Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imelitaka Shirika la Reli Tanzania, TRC, kuhakikisha vijana wananufaika zaidi na mradi wa uundaji na ukarabati wa vichwa vya treni za MGR unaoendelea katika karakana ya Pugu jijini Dar es Salaam.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mbunge Selemani Kakoso, wakati wa ziara ya kamati kukagua maendeleo ya mradi huo Machi 14, 2026.
Kakoso amesema vijana wanaoshiriki katika mradi huo wanapaswa kuendelezwa kwa kupewa mafunzo ya kitaalamu ndani na nje ya nchi ili kuongeza ujuzi, ubunifu na ufanisi katika sekta ya reli.
Kwa mujibu wa TRC, mradi huo tayari umefungua fursa za ajira kwa vijana 34 pamoja na kutoa nafasi kwa wafanyabiashara wa ndani kusambaza vifaa mbalimbali vinavyotumika katika uundaji wa vichwa vya treni.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)