#HABARI: Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ndugu Ado Shaibu, amekutana na kufanya mazungumzo na wanafunzi wa vyuo vikuu wanaotoka wilayani Tunduru katika kikao kilichofanyika jana Machi 14, 2026, jijini Dodoma.
Katika mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Ulanga Annex, Ndugu Ado amewashirikisha vijana hao mikakati na fursa mbalimbali za kimaendeleo zinazotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ili kuwajengea uelewa wa hali ya jimbo lao.
Wakati wa kikao hicho, Ndugu Ado amewahimiza wanachuo hao kutumia elimu yao kushiriki kikamilifu katika ajenda ya kuiboresha Tunduru kwa kutoa mawazo na vitendo.
Mbunge huyo amesikiliza kwa kina maoni na mapendekezo ya wanafunzi hao kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili wilaya hiyo, akisisitiza kuwa mchango wa wasomi ni nguzo muhimu katika kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa Tunduru.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.