‎#HABARI: Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuweka mkazo katika kujenga uchumi jumuishi unao wajumuisha wanawake na vijana kikamilifu katika shughuli za maendeleo.

‎Aidha, imechukua hatua mbalimbali za kisera na kiutendaji ili kuimarisha ushiriki wa wanawake katika shughuli za kiuchumi na kutaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa aslimia 30 ya zabuni za manunuzi ya umma zinatengwa kwa ajili ya makundi maalum ikiwemo wanawake vijana na watu wenye mahitaji maalum hatua iliyofungua fursa kubwa kwa wanawake kushiriki kikamilifu katika zabuni za Serikali jambo linalosaidia kuongeza kipato pamoja na kukuza biashara zao.

‎Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga, jijini Dar es Salaam katika sherehe za miaka 20 ya Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) iliyohusisha ugawaji wa tuzo za Viwanda na Biashara kwa wanawake Wajasiriamali.

‎Amesema kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita TWCC imeendelea kuwa jukwaa muhimu la kukuza ujasiriamali wa wanawake na kuimarisha ushiriki wao katika maendeleo ya kiuchumi ya nchini.

‎Amesema hivi karibuni Serikali ilitekeleza mpango wa kutoa bilioni 200 kwa ajili ya mikopo ya wanawake na vijana ili kuongeza ajira na kukuza ujasiriamali katika makundi hayo muhimu ya jamii.

‎Kwa upande wake Rais wa TWCC CPA Mercy Sila, amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha mazingira ya biashara, akibainisha kuwa maboresho ya Serikali katika upatikanaji wa mitaji kupitia madirisha ya wanawake benki na mifuko ya uwezesheji yamepunguza changamoto za masoko na fedha zilizokuwa zikiwakabili.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *