Programu ya Samia Ubora Kliniki ni mpango maalum wa Serikali ulioan­zishwa ndani ya siku 100 za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Mpango huu unaratibi­wa na Wizara ya Viwanda na Biashara na kutekelez­wa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), kwa lengo la kuwawezesha wajasiri­amali wadogo na wa kati kuzalisha bidhaa bora na salama zinazokidhi viwan­go vya kitaifa na kimataifa, huku ukilinda usalama wa wananchi.

Akizungumza kuhusu kuanzishwa na utekelezaji wa programu hiyo, Mku­rugenzi Mkuu wa TBS, Dkt Ashura Katunzi, anase­ma mpango huo umeleta mabadiliko makubwa kwa wajasiriamali na kwa soko la bidhaa nchini.

“Samia Ubora Kliniki ilianzishwa ili kusogeza huduma za viwango na ubo­ra karibu na wajasiriamali. Lengo letu ni kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa nchini zinakuwa sala­ma, bora na zenye ushindani katika masoko ya ndani na nje ya nchi na kupitia mpango huu, tunawalinda walaji na waka­ti huo huo tun­awajengea uwezo wajasiriamali kukuza biashara zao kwa kuzingatia viwango vya ubora,” anasema Dkt Katun­zi.

Kupitia Samia Ubora Kliniki, TBS imetoa mafunzo bure kwa waja­siria­mali 1,059 katika mikoa 15 nchini. Mafunzo hayo yali­husu uzalishaji wa bidhaa bora, ufungashaji sahi­hi, uongezaji thamani wa bidhaa pamoja na masuala ya masoko. Idadi kubwaya walionufaika ni vija­na, jambo linaloonesha dhamira ya Serikali katika kuwawezesha kiuchumi.

Dk Katunzi anafafanua kuwa, ili kulinda usala­ma wa walaji, TBS ilipima sampuli 800 za bidhaa za wajasiriamali bila mali­po katika maabara zake. Bidhaa zilizokidhi viwango zilipewa Alama ya Ubora ya TBS, hatua iliyowaweze­sha wananchi kuzitambua kwa urahisi na kuzitumia kwa uhakika.

Aidha, bidhaa 192 zil­itunukiwa vyeti vya ubora bila wajasiriamali kulip­ia gharama za ukaguzi na upimaji, na hivyo kufun­gua milango ya masoko ya ndani na nje ya nchi.

Dkt Katunzi anaende­lea kusema kuwa katika kusogeza huduma karibu na wana­nchi, TBS imeanza ujenzi wa majengo ya maabara na ofisi za kanda katika mikoa ya Dodoma, Mwanza na Arusha. Ujenzi wa jengo la Dodoma umefikia zaidi ya asilimia 90, huku jengo la Mwanza likiwa asilimia 70. Kukamilika kwa majengo hayo kutapunguza muda na gharama za kupata huduma za upimaji na uth­ibitishaji wa ubora.

Meneja wa Kanda ya Kati wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Hamis Sudi akizungumza na wananchi wa Itigi mkoani Singida wakati wa utoaji elimu kwa wafanyabiashara wa vyakula na vipodozi.

“Hatua hii ya ujenzi wa maabara itasaidia kusoge­za huduma karibu na wana­nchi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa majibu ya vipimo vya sampuli kwa wakati,” anasema Dkt Katunzi.

Kwa upande wa matumizi bora ya nishati, TBS ime­anzisha maabara maalum ya kupima ufanisi wa matumizi ya umeme kwa vifaa kama majokofu, viy­oyozi, taa, runinga na feni. Hatua hii inalenga kupun­guza gharama za umeme kwa wananchi na kulinda mazingira.

Pia, Shirika limeende­sha warsha 18 kwa waja­siriamali katika sekta za chakula, ujenzi, nishati safi, madini na vifungashio ili kuongeza uelewa kuhu­su umuhimu wa kuzingatia viwango vya ubora.

Dkt Katunzi anaelezea, Utekelezaji wa Samia Ubora Kliniki unafanyika kwa ushirikiano wa taas­isi zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ambazo ni SIDO, BRELA, TANTRADE, TIRDO na Tume ya Ushindani (FCC), hatua iliyowezesha waja­siriamali kupata huduma mbalimbali kwa pamoja kupitia mfumo mmoja.

Mmoja wa wanufaika wa mpango huo, Charles Thomas, mjasiriamali wa usindikaji wa unga lishe kutoka Dar es salaam, anaeleza namna Samia Ubora Kliniki ilivyobadili­sha biashara yake.

“Kabla ya Samia Ubora Kliniki, sikuwa na uelewa wa viwango wala ufun­gashaji sahihi. Niliku­wa nauza bidhaa zangu kwenye soko la kawaida tu, ila baada ya kupata mafun­zo na cheti cha ubora bure kutoka TBS, bidhaa zan­gu sasa zinauzwa kwenye maduka makubwa na map­ato yangu yameongezeka,” anabainisha.

Mafanikio ya Samia Ubo­ra Kliniki ndani ya siku 100 yanaonesha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kujenga uchumi wa viwanda unaozingatia ubo­ra wa bidhaa na usalama wa walaji. Kupitia mpango huu, wajasiriamali wame­pata ujuzi, masoko na vyeti vya ubora, huku wananchi wakinufaika kwa kupata bidhaa salama na bora.

Programu hii inaunga mkono utekelezaji wa Sera ya Viwanda, Ilani ya Uch­aguzi ya Chama Cha Map­induzi (CCM) pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kwa lengo la kuonge­za ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na kimataifa na kuboresha maisha ya wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *