
Mapigano makali yamezuka mapema Jumatano, kati ya waasi wa AFC/M23 dhidi ya Wazalendo katika mji wa Shoa, ulioko katika eneo la Osso Banyungu eneo la Masisi huko Kivu Kaskazini nchini DRC.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari, milio ya silaha nzito na nyepesi imesikika tangu alfajiri, ikiashiria kukithiri kwa mapigano yanayoendelea.
Hali ya taaruki imesababisha wasiwasi mkubwa miongoni mwa raia katika eneo hilo.
Kulingana na vyanzo vya ndani, mashambulio hayo yalianzishwa na waasi wa AFC/M23 wanaotaka kurejesha udhibiti wa eneo hili la kimkakati.
Shambulio hili ni sehemu ya mkakati mpana wa kupanua maeneo yao ya ushawishi katika eneo la Masisi, ambalo limekuwa likikumbwa na ukosefu wa usalama unaoendelea kwa miezi kadhaa.
Hadi Kufikia sasa, hakuna idadi rasmi imeripotiwa kuhusiana na waliojeruhiwa wala kupoteza maisha, hata hivyo, kuzuka upya kwa mapigano kunazua hofu ya kuhama zaidi kwa watu katika eneo hili la Kivu Kaskazini, ambalo tayari limeathiriwa pakubwa na vita.