#HABARI: Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Bagamoyo, Baba Askofu Stephano Lameck Musomba, amekemea tabia ya kuzorota kwa maadili na kupotea kwa utu katika jamii.
Akihubiri wakati wa Ibada katika Parokia ya Bikira Maria wa Mlima wa Karmeli, Bunju jijini Dar es Salaam, Askofu Musomba amesema mwenendo huo unaashiria uwepo wa tatizo la kijamii linalohitaji mjadala wa kina na suluhisho la pamoja.
Ametoa wito kwa wananchi kukuza utamaduni wa mazungumzo, kuvumiliana na kufuata njia halali katika kudai haki ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima.
Askofu Musomba pia ameonya kuhusu kuongezeka kwa imani na vitendo vya kishirikina, akisema endapo vitaachwa kuenea vinaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii siku zijazo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
(Feed generated with FetchRSS)