NAIBU Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dk. Festo Dugange amesema Serikali imetenga shilingi milioni 165.5 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa barabara ya kwa Mwarabu.

Akijibu swali bungeni mjini Dodoma, Dk. Dugange  amesema katika utekelezaji wa awamu ya kwanza ya ujenzi itahusisha ujenzi wa mita 200 kwa kiwango cha zege. Aidha, ameongezea kuwa Serikali itaendelea kutenga fedha nyingine kwa ajili ya kukamilisha mradi huo.

Barabara ya Kilungule inajumuisha eneo la kwa Mwarabu katika Manispaa ya Temeke na inaurefu wa kilomita 0.88. Kwa muda sasa, barabara ya Kwa mwarabu  imekuwa  na changamoto ya kutuama kwa maji  hasa katika kipindi cha mvua na hivyo kupelekea barabara hiyo kutopitika. SOMA: Serikali kuimarisha shule jumuishi, yakataza tozo holela

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *