Taifa litapata vipaji Mac D marathon – NgokaTaifa litapata vipaji Mac D marathon – Ngoka

DAR ES SALAAM: Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam (DAA),  Amani Ngoka amesema kupitia mbio za ‘Mac D’ taifa linategemea kupata vipaji vipya kwa ajili ya mashindano mbalimbali ya kimataifa hapo baadaye.

Mbio za ‘Mac D’ zitafanyika Julai 04, 2026 katika viwanja vya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Kunduchi jijini Dar es Salaam.

Amani Ngoka amezungumza hayo katika uzinduzi wa mbio hizo uliofanyika leo Aprili 9, jijini Dar es Salaam ambapo lengo ni kuiunga mkono serikali matumizi ya nishati safi.

“Mbizo hizi zina malengo ya baadaye kwa ajili ya manufaa ya Tanzania,” amesema Ngoka.

Akizungumzia mbio hizo, Mkurugenzi wa Mipango Mac D, Denzel Rweyunga amesema mbio zitahusisha washiriki wa Km 5, Km 10, na Km 21, lakini pia tutakuwa na mbio kwa ajili ya watoto.

“Tunatamani kuona wazazi wakiwa na watoto, maana tutakuwa na mbio za kilomita mbili kwa ajili ya watoto,” amesema Rweyunga.

Aidha, amesema dirisha la usajili limeanza rasmi kuelekea mbio hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *