Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imetenga zaidi ya shilingi bilioni 5.7 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo masoko, kwa lengo la kutoa fursa za ajira na kujiajiri kwa vijana.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema hayo wakati wa uzinduzi wa jukwaa la Vijana Platform, akibainisha kuwa miongoni mwa fursa zitakazotolewa ni ujenzi wa masoko ya wamachinga katika maeneo ya Jangwani, Gongo la Mboto na Zingiziwa ndani ya jiji hilo.

#AzamTVupdates
✍Upendo Michael
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *