
WAZIRI MKUU, Dk Mwigulu Nchemba, amemwagiza mkandarasi anayejenga uwanja wa Mashindano ya Mataifa ya Afrika(AFCON)2027 ahakikishe mradi huo unakamilika kwa wakati.

Ujenzi wa uwanja huo unaojengwa katika kata ya Olomoti, jijini Arusha ni sehemu ya maandalizi ya Mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, yakayofanyika kwenye nchi tatu za Tanzania, Kenya na Uganda.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa uwanja huo, Waziri Mkuu amemuagiza mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha kuwa ujenzi unakamilika kwa wakati na kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.