SAKATA la mshambuliaji Jonathan Sowah limechukua sura mpya baada ya nyota huyo kutoonekana katika mazoezi ambayo alitakiwa na mabosi wake kuyafanya na timu ya vijana U20.

Simba wiki moja iliyopita ilitoa msimamo wake juu ya sakata la Sowah, ikisema itampiga faini ya fedha kwa makosa ambayo alikiri kuyafanya tangu kusimamishwa, pia ikimtaka kwenda kufanya mazoezi na timu ya vijana ya wekundu hao.

Ilitaka Sowah kufanya mazoezi na timu ya vijana, ili kuangalia mabadiliko ya nidhamu ya mshambuliaji huyo raia wa Ghana, aliyesajiliwa msimu huu akitokea Singida Black Stars.

Taarifa za ndani zililiambia Mwanaspoti, katika mazoezi ya timu ya vijana ya Simba, Sowah hajahudhuria kwa siku ya pili hadi jana, huku akiwa hajatoa taarifa yoyote kwa makocha ambao walitakiwa kumpokea.

SOW 01

Mazoezi hayo ambayo yalianza juzi kwenye uwanja mmoja wa jeshi, Sowah hakufika, lakini jana tena hakutokea huku makocha hao wakipeleka kila mrejesho juu ya mahudhurio yake.

“Huku Sowah hajafika, tulianza jana (juzi) hatukumwona na hata leo (jana) hajafika tena, sisi kazi yetu ni kuwapa taarifa viongozi kama akifika au hata kama hajafika,” amesemammoja wa wasimamizi wa mazoezi hayo ya timu ya vijana.

“Wakati wanasema viongozi walishatupa mpaka namba zake na wamesemayeye pia wamempa mawasiliano ya kocha Bocco (John), huko kote hakuna ambaye anajua lolote wala hakuna ambaye amempigia.”

SOW 02

UPANDE WA SOWAH

Wakati hali ikiwa hivyo, taarifa kutoka kwa wasimamizi wa Sowah inaelezwa kwamba mshambuliaji huyo hayupo tayari kufanya mazoezi na timu hiyo ya vijana, akiona hakuna ambako aliikosea klabu hiyo.

“Hawa Simba ni kama hawamtaki Sowah, sasa wanamtafutia sehemu ya kumalizana naye bila kujiingiza matatizoni na Fifa, Sowah mwenyewe ameshasema hataenda huko kwenye mazoezi ya vijana,” amesemammoja wa marafiki na wasimamizi wa mshambuliaji huyo.

Simba ilimsimamisha Sowah kwa takribani wiki nne kabla ya baadaye kuja na msimamo huo, ikiwa ni baada ya mshambuliaji huyo kujieleza kwa uongozi wa klabu hiyo kwenye kamati ya nidhamu ya wekundu hao.

SOW 03

WASIKIE SIMBA

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally, amesemaSowah alitakiwa awe na timu ya vijana kwa ajili ya kufanya mazoezi, ikiwa ni sehemu ya kutumikia adhabu yake.

“Ni kweli alitakiwa awe na timu ya vijana ikiwa ni sehemu ya kutumikia adhabu yake na ni sehemu ya kuangalia kama ana mabadiliko.

“Bado sijajua atakuwa huko kwa muda gani kwa sababu ni kipindi cha maangalizo, kwa hiyo ikitoka ripoti kuwa ameimarika basi atarudi moja kwa moja timu ya vijana kuendelea kutumikia mkataba wake,” amesemaAlly.

Sowah alisaini mkataba wa miaka miwili ambapo huu ni msimu wake wa kwanza akitokea Singida Black Stars ambako alitumika kwa miezi sita pekee kabla ya kutua Simba.

Msimu huu katika ligi ana rekodi ya kucheza mechi nne sawa na dakika 247, akiwa amefunga mabao matatu, huku Singida akimaliza na mabao 13 msimu uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *