#HABARI: Kampuni ya GASCO, ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), imeendelea kuwa kinara katika kuwawezesha Watanzania wazawa kwa kuwapa nafasi za moja kwa moja kwenye miradi ya uchakataji na usambazaji wa gesi asilia.
Hatua hiyo imetajwa kuwa mhimili wa kukuza ajira na ujuzi nchini, ikihusisha uendeshaji wa mitambo muhimu katika maeneo ya Songosongo, Somangafungu, Madimba, na Kinyerezi.
Akizungumza katika maadhimisho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) mkoani Njombe, Afisa Mazingira Mwandamizi wa GASCO, Bw. Sanisha Kigadye, ameeleza kuwa kampuni hiyo inaendeshwa na wataalamu wazawa wenye weledi wa hali ya juu.
Mafanikio haya ni matokeo ya uwekezaji mkubwa katika rasilimali watu, ambapo Watanzania sasa wanasimamia nyanja za uhandisi, matengenezo ya mitambo, na uhifadhi wa mazingira bila utegemezi wa nje.
Aidha, miradi hiyo imefungua milango kwa vijana kupata mafunzo kwa vitendo (internship) na ajira za kudumu, jambo linalosaidia kujenga kizazi kipya cha wataalamu wabobezi katika sekta ya nishati.
Mchango wa GASCO unaendelea kuleta matokeo chanya kwa kuimarisha uchumi wa taifa na kuhakikisha kuwa rasilimali za ndani zinatumika kwa manufaa ya Watanzania wote kupitia usimamizi wa wazawa wenyewe.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)