Wakati shinikizo la wanajihadi likiongezeka katika eneo la Sahel, serikali ya Burkina Faso imepitisha muswada Aprili 24 wa kuunda kikosi cha wanajeshi wa akiba 100,000. Baraza la kijeshi linatoa wito kwa “raia wote wenye umri wa kupigana kuilinda” Burkina Faso kujiunga na jeshi. Tangazo hili, katika utekelezaji wake ujao, linasababisha wasiwasi miongoni mwa watetezi wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na Human Rights Watch.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Shirika la kimataifa la Haki za binadamu, Human Rights Watch (HRW), ambalo wiki tatu zilizopita illichapisha ripoti ya kutisha kuhusu dhuluma na uhalifu uliofanywa na jeshi na wasaidizi wake wa VDP, linaona tangazo hili la Waziri wa Vita wa Burkina Faso, Jenerali Simporé, linatia wasiwasi.

Kuajiri wanajeshi 50,000 wa zamani ambao hapo awali walikuwa wamekamilisha kazi yao ya kijeshi, pamoja na wanafunzi wengine 50,000 wapya ambao watahitaji kufunzwa katika sanaa ya vita, ni ishara mbaya, kulingana na Human Rights Watch. Hili linatia wasiwasi hasa ikizingatiwa kwamba, ingawa Ouagadougou inaajiri watu kwa dharura, mashirika ya usaidizi wa haki za binadamu ambayo hapo awali yaliwafunza wanajeshi na VDP (watu wanoajitolea kwa ajili ya ulinzi wa nchi) yamesitisha shughuli zote nchini Burkina Faso.

Hili, kulingana na Human Rights Watch, linatia shaka kubwa kuhusu uwezo wa utawala wa kijeshi wa kupunguza dhuluma zitakazofanywa na kikosi hiki kinachoibuka. Unyanyasaji kama huo, katika vita vinavyoendelea nchini Burkina Faso, ni mwingi na umesababisha kuuawa kwa raia 1,800 kati ya mwaka 2023 na 2025. Theluthi mbili ya waathiriwa hawa 1,800 waliathiriwa si na magaidi, bali na vikosi vya jeshi vya Burkina Faso ambavyo vilikuwa vimejiandaa vyema kwa mapigano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *