Vita vya Mashariki ya Kati: Israel yapanua operesheni za kijeshi nchini LebanonVita vya Mashariki ya Kati: Israel yapanua operesheni za kijeshi nchini Lebanon

Angalau watu 19 wameuawa nchini Lebanon katika mashambulizi ya anga ya Israel katika kipindi cha saa 24 zilizopita, siku ya mwisho ya usitishaji mapigano, ambayo iliongezwa kwa siku 45 wakati wa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Lebanon na Israel huko Washington siku ya Alhamisi, Mei 14, na Ijumaa, Mei 15.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Israel lilifanya mashambulizi kadhaa siku ya Jumapili dhidi ya miji iliyo kusini mwa Lebanon, huku Hezbollah ikizidisha mashambulizi yake kwenye uwanja wa vita wa Lebanon na kaskazini mwa Galilaya.

Siku ya mwisho ya makubainao ya usitishaji mapigano yaliyoongezwa muda kwa siku 45, jeshi la Israel lilipanua wigo wa operesheni zake na kuongeza mashambulizi yake katika maeneo kadhaa ya Lebanon, anaripoti mwandishi wetu huko Beirut, Paul Khalifeh. Ndege za kivita, ndege zisizo na rubani, na vifaru vilishambulia miji na vijiji takriban 30 kaskazini mwa Mto Litani na kusini mwa Bonde la Bekaa mashariki mwa Lebanon siku nzima.

Kulingana na ripoti ya awali kutoka Wizara ya Afya, watu watatu walifariki huko Tayr Felsay na wawili huko Tayr Debba, ikiwa ni pamoja na mtoto mmoja katika kila mji. Karibu watu 15 walijeruhiwa katika mfululizo wa mashambulizi, wizara iliongeza. Hapo awali, maeneo ya Nabatieh na Tyre yalilengwa na mashambulizi, pamoja na mji wa Sohmor katika Bonde la Bekaa mashariki mwa Lebanon, kulingana na shirika la habari la serikali la Lebanon, ANI.

Jeshi la Israel linaendelea na sera yake ya kuondoa watu Kusini kwa kuwaamuru wakazi wa vijiji tisa kuhama makazi yao. Vijiji vinne kati ya vilivyoathiriwa viko katika wilaya ya Saida, ambayo hadi sasa ilikuwa imeepushwa mapigano yanayoendelea.

Jeshi la Israeli pia lilijaribu kupenya kaskazini mwa Litani kwa mara ya pili katika wiki moja. Wanajeshi kadhaa walijeruhiwa katika jaribio hili la uvamizi, lililofanyika katika eneo la kati la kusini mwa Lebanon.

Hata hivyo, Marekani ilitangaza siku ya Ijumaa, wakati wa siku ya pili ya mazungumzo kati ya Israel na Lebanon huko Washington, kuongezwa kwa muda wa siku 45 ya makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yalianza kutekelezwa Aprili 17 na yalipaswa kumalizika siku ya Jumapili hii. Hezbollah inakataa mazungumzo , ya kwanza tangu miongo kadhaa kati ya nchi hizo mbili, ambazo hazidumishi uhusiano wa kidiplomasia. Wanahusu hasa suala gumu la kupokonya silaha kundi hilo, ambalo inapinga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *