#HABARI: Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Jukwaa la Uwekezaji Zanzibar 2026 limefanikiwa kufungua fursa mpya, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, na kuchochea ukuaji wa uchumi wa visiwa hivyo.
Dkt. Mwinyi, amewahakikishia wawekezaji kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara kupitia uwazi na mageuzi ya kisekta.
Pia Dkt. Mwinyi ameipongeza Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) kwa kuandaa jukwaa hilo lililokusanya washiriki zaidi ya 600 duniani na kuitangaza Zanzibar kama kitovu cha uwekezaji.
Katika hafla hiyo, ZIPA ilimtunuku Rais Mwinyi Tuzo Maalum ya Uongozi kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuendeleza sekta ya uwekezaji.
Katika hatua nyingine, Rais Mwinyi alikutana na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) na kuwahimiza kuchamkia fursa za kuwekeza nyumbani.
Aliwaomba kutumia mitaji, maarifa, na ujuzi wao kuchangia kwa dhati katika maendeleo ya kiuchumi ya taifa lao.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)