#MICHEZO: Mwamuzi kutoka Somalia, Omar Abdulkadir Artan, amerejea nyumbani kwao Mogadishu na kupokelewa kwa heshima kubwa na wananchi pamoja na mashabiki wa soka.
Omar Artan hakupata nafasi ya kuchezesha michuano ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kunyimwa idhini ya kuingia nchini Marekani, jambo lililomaliza ndoto yake ya kihistoria ya kuiwakilisha Somalia katika moja ya mashindano makubwa zaidi ya mpira wa miguu duniani.
Hata hivyo, hatua yake haikuishia hapo, kwani mamlaka za soka nchini Canada zimethibitisha kumkaribisha ili kuchezesha mechi zitakazofanyika Vancouver, hatua inayompa nafasi mpya ya kuendeleza taaluma yake ya uamuzi.
Licha ya changamoto alizokutana nazo, mapokezi aliyopata Mogadishu yameonesha heshima kubwa na upendo kutoka kwa mashabiki na wananchi waliothamini mchango wake katika soka.
Wachambuzi wanasema Omar Artan sasa anaendelea kujijenga upya katika jukwaa la kimataifa baada ya kupata nafasi mpya Canada.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
(Feed generated with FetchRSS)