Ndege za Marekani za kuongeza mafuta angani (refuelling aircraft) zimehamishiwa katika eneo la Palestina inayokaliwa, kutokana na hofu ya mashambulizi yanayoweza kufanywa na Iran.

Hatua hiyo inatajwa kuwa imechukuliwa kwa lengo la kuimarisha tahadhari za kiusalama na kulinda rasilimali za kijeshi za Marekani katika eneo hilo.

Ripoti zinasema kuwa, kufuatia kile kilichoelezwa kuwa ni mapigo makali ya Iran, ndege za Marekani za kuongeza mafuta angani zimehamishiwa katika Palestina inayokaliwa, hatua inayotajwa na baadhi ya vyanzo kuwa ni ishara ya kurejea nyuma Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) kutokana na hofu ya mashambulizi ya Iran.

Afisa mmoja wa kijeshi, katika mahojiano na chombo cha habari cha Defa Press, amesema kuwa mashambulizi makubwa ya vikosi vya jeshi la Iran dhidi ya Marekani katika siku zilizopita yamesababisha uharibifu wa baadhi ya ndege za Marekani za kuongeza mafuta angani.

Afisa huyo amesema kuwa shambulio lililofanywa usiku wa Ijumaa na vikosi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya vituo vya Marekani katika kambi ya Al Udeid nchini Qatar, Al-Kharj nchini Saudi Arabia na Al-Azraq nchini Jordan, lilisababisha baadhi ya ndege hizo kuharibiwa au kupata madhara.

Ameongeza kuwa hatua ya kuhamisha ndege hizo imekuja kutokana na hofu ya mashambulizi zaidi katika eneo hilo.

Kufuatia tukio hilo, makamanda wa jeshi la Marekani wamechukua hatua ya kuhamisha baadhi ya ndege za kuongeza mafuta angani ambazo hazikuharibiwa katika mashambulizi, na kuzipeleka katika Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion uliopo katika maeneo ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Iran imefanikiwa, katika siku za hivi karibuni, kutekeleza mashambulizi yenye ufanisi na makali dhidi ya vikosi na vifaa vya kijeshi vya Marekani katika kambi za kijeshi za Washington zilizopo Asia Magharibi, zikiwemo kambi zilizopo Kuwait, Qatar, Bahrain na Jordan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *