Kesi ya uhaini inayomkabili mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema, Tundu Lissu, imeanza kusikilizwa Jumatatu wiki hii katika mahakama kuu ya Dar es Salaam, ambapo upande wa mashtaka umeanza kuwasilisha ushahidi wao.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kesi hii imeanza ikiwa zimebaki takribani siku 24 kabla ya raia wa nchi hiyo kupiga kura katika uchaguzo mkuu wa rais, wabunge na madiwani, Oktoba 29.

Kabla ya kuanza kwa kesi hiyo, Tundu Lissu aliwasilisha mapingamizi kadhaa ikiwemo hati ya ratiba ya kesi itakavyoendeshwa na kumalizika Novemba 12, pingamizi ambalo hata hivyo majaji wanaosikiliza shauri lake wamelitupilia mbali kwa kile wamesema ratiba hiyo haiwabani kumaliza tarehe tajwa au kabla.

Baada ya uamuzi mdogo kuhusu mapingamizi yake kutolewa, upande wa Jamhuri ulimleta shahidi wa kwanza kutoka idara ya upelelezi ya polisi, ambapo ameieleza mahakama namna walivyochunguza picha mjongeo iliyomuonesha Lissu akitoa maneno ya kuhamasisha uasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *