Wananchi wa Italia na waungaji mkono wa Palestina wametoa wito wa kuufutwa mechi ya soka kati ya Italia na utawala ghasibuu wa Israel wakilalamikia mauaji na jinai za israel dhidi ya Wapalestina katika Uukanda wa Gaza.

Meya wa Udine mji ambao umepangwa kuchezwa mechi hiyo Oktoba 14 amesema kuwa, haungwi mkono mechi hiyo kuchezwa katika mji huo na ametaka kuakhirishwa kwa mchezo huo.

Mechi ya Israel na Italia ya kufuzu Kombe la Dunia wiki ijayo inatarajiwa kuvutia waandamanaji wengi wanaoiunga mkono Palestina nje ya uwanja wa soka huko Udine kuliko watazamaji waliokata tiketi ndani ya uwanja. “Kutakuwa na watu 10,000 nje ya uwanja wanaopinga mechi hiyo wakilalamikia jinai za Israel Gaza na 5-6,000 ndani ya uwanja watakaokuwa wakitazama mechi hiyo.”

Waandamanaji tayari walikaribia lango la kituo cha mazoezi cha Italia huko Florence wiki iliyopita kutaka mechi hiyo isichezwe kwa sababu ya vita huko Gaza — sehemu ya mgomo wa kitaifa ambao ulishuhudia mamilioni ya wanaharakati wakiingia mitaani.

Hayatakuwa mazingira tulivu,” kocha wa timu ya taifa ya soka ya Italia Gennaro Gattuso alikiri Jumanne kutoka ndani ya kituo cha mazoezi cha Coverciano ambacho kililengwa.

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Italia sambamba na kuonyesha kusikitishwa na kile kinachojiri Gaza,  amesema, “Ninaelewa hilo, naelewa wasiwasi wa watu kuhusu hali hii, lakini tunajua tunapaswa kucheza mchezo huu, kwani tukisusia Israel itapatiwa pointi tatu, na hiki ni kitu ambacho hatutaki kwani ushindi katika mechi hii ni muhimu kwa ajili ya harakati zetu za kuelekea kufuzu Kombe la Dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *