Waziri Mkuu wa China Li Qiang anazuru Pyongyang leo Alhamisi , Oktoba 9, kwa ziara rasmi ya “nia njema”, kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya China. Li Qiang atahudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 80 ya Chama cha Wafanyakazi siku ya Ijumaa, na hivyo kumfanya kuwa afisa wa ngazi ya juu zaidi wa China aliyeitembelea nchi hiyo tangu mwaka 2019. Hii ni ishara ya kuimarika kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ziara hii inaimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili ikilinganishwa na uhusiano wa kisiasa wa China na Korea Kaskazini katika kipindi cha kabla ya UVIKO-19. Lakini kuimarika kwa hali hii ya kisiasa kumeanza wiki chache zilizopita, kulingana na Théo Clément, mtafiti mshiriki katika EHESS.

“Hii inaendana na picha za kuvutia tulizoziona Beijing wakati wa gwaride kubwa la kijeshi lililoandaliwa nchini China, ambapo Xi Jinping, Kim Jong-un, na Putin walionekana kuwa washirika kwenye jukwaa la Tianamento Square,” mtafiti anakumbusha.

Lakini ziara hii inaweza kusaidia kutatua baadhi ya mambo yanayoshikamana katika uhusiano kati ya China na Korea Kaskazini, ambayo mpaka wake bado umefungwa kwa Beijing.

Maelewano ya Kiuchumi

“Kuna dalili kadhaa zinazoonyesha kwamba China ina nia kubwa ya kujihusisha tena kiuchumi na Korea Kaskazini, lakini Korea Kaskazini inajizuia kidogo. Nadhani Pyongyang inataka kuifahamisha China kwamba inatarajia masharti mengi ya kibiashara yenye manufaa zaidi, na nadhani ziara ya Waziri Mkuu wa China nchini Korea Kaskazini inaweza kuwa sehemu ya mazungumzo haya,” anaeleza Théo Clément.

Wakati wa ziara hii, Korea Kaskazini inaweza kusukuma uhusiano sawa na ule Pyongyang inayo na Urusi, ambayo inaweza kumaanisha mambo mawili kwa Beijing: uhamisho zaidi wa teknolojia na heshima kwa uhuru wa kiuchumi wa Korea Kaskazini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *