Baada ya tangazo la Israel na Hamas, kukubali mkataba wa kusitisha vita uliopendekezwa na Marekani, Wapalestina wamekuwa wakisherehekea, kuanzia Jumatano usiku hadi Alhamisi kusini mwa mji wa Khan Younis, na maeneo mengine huko Gaza.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mjini Tel Aviv, raia wa Israeli ambao wapendwa wao wametekwa na Hamas, nao pia wamekuwa wakisherehekea hatua hiyo, wakionesha matumaini ya kuonana na wapendwa wao.

Israeli na Hamas wamekubaliana kuhusu utekelezwaji wa awamu ya kwanza ya mkataba huo, ambapo Hamas watawaachia huru mateka wote waliotekwa Israeli ndani ya siku kadhaa zijazo, huku Israeli ikiwaachia wafungwa elfu mbili wa Kipalestina.

Raia wa Palestina akiwa kando la hema lake baada ya Rais Trump kutangaza usitishaji wa vita Gaza.
Raia wa Palestina akiwa kando la hema lake baada ya Rais Trump kutangaza usitishaji wa vita Gaza. REUTERS – Ramadan Abed

Israel nayo  inatarajiwa kuwaondoa wanajeshi wake Gaza na kupelekwa katika eneo lililokubaliwa, katika utekelezwaji wa mkataba huu unaotarajiwa kumaliza vita vya miaka miwili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *