Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar bin Zubeir Ali amewataka Waislamu na Watanzania kwa ujumla kuhubiri na kulinda amani ya nchi, akisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa Uislamu na maendeleo ya taifa.

Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa dini mjini Makambako, Mufti Abubakar amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, 2025, na kuwachagua viongozi watakaodumisha utulivu na mshikamano.

Amesema Mtume Muhammad (S.A.W.) alikuwa mtume wa amani, hivyo kila Muislamu anapaswa kuwa mfano wa kuigwa katika kudumisha upendo, utulivu na umoja wa taifa.

✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *