Idadi kubwa ya wakazi hao wa Gaza walitumia njia hiyo ya kaskazini kuelekea Gaza City, mji mkubwa wa eneo hilo ambao umekuwa chini ya mashambulizi makubwa siku chache zilizopita .

Wakazi wa Gaza waonywa kutoingia maeneo yanayodhibitiwa na jeshi la Israel

Msemaji wa jeshi la Israel brigadia jenarali Effie Defrin, amewataka wakazi wa Gaza kuepuka kuingia katika maeneo yalio chini ya udhibiti wa Israel.

Wakati huo huo, mjumbe maalum wa Marekani katika Mashariki ya Kati Steve Witkoff, amesema jeshi hilo limekamilisha awamu ya kwanza ya kujiondoa Gaza na kipindi cha kuwaachilia mateka kimeanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *