#HABARI: Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuwa vita vya Gaza vimekwisha huku akielekea Mashariki ya Kati, ambako atalihutubia Bunge la Israel (Knesset) na kuongoza kwa pamoja mkutano wa kilele nchini Misri kuhusu makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas.
Hamas imewakabidhi wafungwa wa Kiaisraeli saba kwa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) huko Gaza, na inatarajiwa kuwaachia wengine 13 zaidi, huku Wapalestina wakisubiri kuachiwa kwa takriban wafungwa 2,000 walioko magerezani nchini Israel.
Watu wa Msalaba Mwekundu wanasimamia mipango ya kubadilishana wafungwa, ikiwemo usafirishaji wa wafungwa wa Kipalestina hadi kituo maalumu cha matibabu kilichoko Khan Younis, kilichoandaliwa ndani ya Hospitali ya Nasser mahsusi kwa siku hii.
Madaktari na wauguzi walioko katika eneo hilo wamesema wako tayari kuwapokea wafungwa hao, ambao watapimwa afya kabla ya kuunganishwa tena na familia zao.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania