Mgombea wa Urais kupitia chama cha ADA–TADEA, Georges Busungu amesema endapo atapata ridhaa ya kuongoza nchi, atatumia siku kumi za mwanzo baada ya kushika madaraka kuhakikisha anatekeleza mambo sita ya msingi, ikiwemo kuunda tume ya kupata katiba mpya, kurekebisha sheria kandamizi, na kufanya mapitio ya shughuli zote za kiuchumi.

Aidha, ameahidi kuweka mazingira yatakayowezesha wananchi kuwa na uhuru kamili wa kutoa maoni.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *