Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 712 kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja mkoani Morogoro kwa kipindi cha miaka minne.
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS ) mkoani humo, Mhandisi John Mkumbo, amesema miradi hiyo imejumuisha ujenzi wa madaraja sita na barabara kuu kama Bigwa–Mvuha, Ifakara–Mbingu na Ubena Zomozi–Ngerengere, sambamba na miradi ya dharura inayofadhiliwa na Benki ya Dunia.
Ameongeza kuwa serikali pia inatekeleza miradi ya usanifu na matengenezo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 26 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ili kuhakikisha mtandao wa barabara wa kilomita 2,071.23 unakuwa imara na unachochea maendeleo ya kiuchumi mkoani humo.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi