‎#HABARI: Serikali imeendelea kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto kwa kuhakikisha wadau wote wenye jukumu la kuhakikisha watoto wanakua na kufikia utimilifu wao.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju wakati akifungua rasmi mafunzo ya kadi ya alama (scorecard) kwa Maafisa Ustawi wa Jamii, Elimu na Lishe pamoja na waratibu wa afya ya Mama na Mtoto kutoka Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini.

Wakili Mpanju amesema kadi hiyo ya alama itawezesha kuunganisha sekta zote na kufanya kazi kwa pamoja hivyo kumlazimu kila mtu kutekeleza majukumu yake kama inavyotakiwa.

“Tumepata nyenzo ya Kitaifa itayoweza kutusaidia kufuatilia mienendo ya mtoto kuanzia ujauzito, kuzaliwa, ukuaji na ulinzi wake mpaka kufikia hatua ya elimu na inaleta sekta zote kwa pamoja na hii si nyenzo ya kawaida” amesema Wakili Mpanju.
Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *