Uhaba wa usafiri wa mabasi kutoka Dar es salaam kwenda mikoa mbalimbali nchini umeilazimu Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) kufungua maombi ya leseni za muda kwa wasafirishaji ili kuongeza idadi ya mabasi kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.
Hatua hii ni baada ya kushuhudiwa kwa idadi kubwa ya wasafiri hasa katika stendi kuu ya mabasi ya Magufuli jijini Dar es salaam.
#AzamTVUpdates
Mhariri | @claud_jm