#HABARI: Mwanga Hakika Bank (MHB) imepewa Tuzo ya Consumer Choice Awards Africa 2025 katika kipengele cha Benki inayotoa huduma za Mikopo Rafiki (Benki za Kati) kupitia mkopo wa Fursa mahususi kwa wajasiriamali wadogo.
Ushindi huu unaangazia dhamira ya Mwanga Hakika Bank katika kuwawezesha wajasiriamali katika kukuza biashara zao kiuchumi kupitia huduma mahususi zinazowagusa moja kwa moja ikiwemo Akaunti ya Fursa kwa ajili ya kujiwekea akiba na Mkopo wa Fursa ambao hutolewa kwa masharti na riba nafuu ili kukuza biashara.
Kupitia huduma hizo, Mwanga Hakika Bank inaendelea kutoa mchango muhimu katika kuwawezesha wajasiriamali wakubwa na wadogo wengi zaidi nchini kufikia malengo yao, kujikimu katika uchumi wa kisasa na kuboresha maisha yao na jamii kwa ujumla.
Tuzo hii ilipokelewa na Mkuu wa Idara ya Wateja Wadogo na wa Kati, Bw. Mwinyimkuu Ngalima katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika jijini Dar wa Salaam hivi karibuni.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania