Serikali imesema imekusudia kunufaisha wananchi milioni 2.85 kupitia mradi wa Mradi wa Mawasiliano ya Simu Vijijini – Awamu ya 10, ambapo Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Kairuki (Mb), amewataka watoa huduma za mawasiliano nchini kuhakikisha wanafikisha mawasiliano vijijini kwa kiwango kinachokubalika.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini mikataba ya utekelezaji wa mradi huo, kati ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na watoa huduma za mawasiliano, Kairuki amesema hatua hiyo ni muhimu, ambapo mradi huo utakuwa wa minara 201 itakagharimu shilingi bilioni 19.7 katika kata 201 zenye vijiji 263.

Imeandaliwa na Abubakar Yusuf.

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *