Serikali inaendelea kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto kwa kuhakikisha wadau wote wenye jukumu la kuhakikisha watoto wanakua na kufikia utimilifu wao.

Hayo yamebainishwa leo 04, Novemba 2025 na Naibu Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju wakati akifungua rasmi mafunzo ya kadi ya alama (scorecard kwa Maafisa Ustawi wa Jamii, Elimu na Lishe pamoja na waratibu wa afya ya Mama na Mtoto kutoka Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini.

Wakili Mpanju amesema kadi hiyo ya alama itawezesha kuunganisha sekta zote na kufanya kazi kwa pamoja hivyo kumlazimu kila mtu kutekeleza majukumu yake kama inavyotakiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *