#HABARI: Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, Bw. Frank Sichalwe, ametoa wito kwa madiwani walioapishwa kutambua kwamba nafasi waliyopewa ni dhamana kutoka kwa wananchi, hivyo wanapaswa kuwatumikia kwa unyenyekevu na kujiepusha na tabia za kujiona wanajua kila kitu. Amesema uongozi bora unahitaji kusikiliza, kujifunza na kushirikiana na wananchi ambao mara nyingi huwa na uelewa mpana kuhusu changamoto zinazowakabili katika maeneo yao.

Bw. Sichalwe ameyasema hayo mara baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwaapisha madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, akisisitiza kuwa cheo si ruhusa ya kudharau, kubeza au kupuuzia maoni ya wananchi. Ameeleza kuwa mara nyingi wananchi wana ujuzi, uzoefu na taarifa muhimu kuhusu maendeleo ya kata zao, hivyo madiwani wanapaswa kushirikiana nao kwa karibu ili kufanikisha majukumu yao.

Ameongeza kuwa madiwani wanalo jukumu kubwa la kusimamia miradi ya maendeleo, kuibua fursa, kuhamasisha uchumi wa eneo na kuhakikisha rasilimali za umma zinatumika ipasavyo. Amehitimisha kwa kuwataka kuonesha mfano wa uadilifu, uwajibikaji na nidhamu ya kazi, ili Halmashauri ya Mbarali iendelee kusonga mbele kwa kasi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *