Serikali ya Marekani imeongeza karibu mara tatu idadi ya nchi ambazo wamiliki wa pasipoti zao watahitajika kuweka dhamana ya hadi dola 15,000 ili kuomba kuingia nchini humo.

Chini ya wiki moja baada ya kuongeza nchi saba kwenye orodha ya mataifa yanayohitaji dhamana za viza, na kufanya jumla kuwa 13, wizara ya mambo ya nje ya Marekani, sasa imeongeza nchi nyingine 25 zaidi.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa kwenye tovuti travel.state.gov, mahitaji ya dhamana kwa nyongeza za hivi karibuni yataanza kutumika Januari 21. 

Hatua hiyo inamaanisha kuwa sasa kuna nchi 38, 23 kati yao zikiwa za Afrika lakini baadhi ziko Amerika ya Latini na Asia, kwenye orodha hiyo, jambo linalofanya mchakato wa kupata viza ya kuingia Marekani umgharimu mtu sana au usiwezekane kwa wengi.

Nchi mpya zitakazohitaji dhamana za viza kuanzia Januari 21 ni: Algeria, Angola, Antigua na Barbuda, Bangladesh, Benin, Burundi, Cape Verde , Cuba, Djibouti, Dominika, Fiji, Gabon, Côte d’Ivoire, Kyrgyzstan, Nepal, Nigeria, Senegal, Tajikistan, Togo, Tonga, Tuvalu, Uganda, Vanuatu, Venezuela na Zimbabwe.

Nchi hizo zinaungana kwenye orodha hiyo na Bhutan, Botswana, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Gambia, Guinea, Guinea-Bissau, Malawi, Mauritania, Namibia, São Tomé na Príncipe, Tanzania, Turkmenistan na Zambia.

Hatua hiyo ni sehemu ya kampeni ya rais wa Marekani, Donald Trump ya kubana masharti ya kuingia nchini humo, ikiwemo kuwataka raia wa nchi zote zinazohitaji viza kuhudhuria mahojiano ya ana kwa ana na kuweka hadharani rekodi za miaka ya ushiriki wao katika mitandao ya kijamii pamoja na maelezo ya kina kuhusu safari zao za zamani na mipangilio yao ya makazi na ya familia.

Maafisa wa Marekani wamekuwa wakiutetea utaratibu wa dhamana, ambao unaweza kuwa kati ya dola 5,000 hadi dola 15,000, wakidai kwamba una ufanisi katika kuhakikisha raia wa nchi zilizolengwa hawabaki ndani ya nchi hiyo zaidi ya muda wa viza zao.

Hata hivyo, kuwalipisha dhamana hiyo hakutoi hakikisho kuwa viza itatolewa, lakini kiasi hicho cha fedha kitarudishwa kwa mhusika ikiwa viza haitatolewa au wakati mmiliki wa viza atakapothibitisha kuwa amefuata masharti yanayotakiwa…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *