Serikali imesema vijana nchini wanapaswa kuendelea kuchangamkia fursa za ajira zinazotafutwa ughaibuni katika taaluma na fani mbalimbali ili kuendelea kunufaika ikiwemo fursa 8,000 mpya ambazo serikali imezitafuta kwenye mataifa mbalimbali ya Ulaya na Falme za Kiarabu.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano ya Kazi), Deus Sangu wakati akiwaaga zaidi ya vijana 100 waliopata ajira katika sekta zaidi ya tatu nje ya nchi.

Imeandaliwa na Robert Mayungu.

Mhariri @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *