Serikali imetangaza kuanza utekelezaji wa mkakati wa kubadilisha miundombinu ya maji isiyofaa, kwa lengo la kudhibiti upotevu wa maji na kuboresha huduma kwa wananchi.

Aidha, wananchi wametakiwa kutunza na kulinda miradi ya maji inayotekelezwa katika maeneo yao ili kuhakikisha uendelevu wa huduma hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maji, Kundo Mathew, wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Mara, ambapo alikagua utekelezaji wa miradi ya maji na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi.

#AzamTVUpdates

✍Augustine Mgendi
Mhariri | @claud_jm

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *