#HABARI: Kamati ya Maadili ya Bodi ya Wakurugenzi ya Ununuzi na Ugavi imependekeza kuchukuliwa kwa hatua kali za kinidhamu dhidi ya wataalamu 14 hapa nchini baada ya kubainika kukiuka taratibu na sheria za manunuzi. Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi, ameeleza kuwa mapendekezo hayo yameshawasilishwa katika mamlaka zao za ajira ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya wataalamu hao waliohusika katika ubadhirifu na ukiukwaji wa miongozo ya kazi zao.

Mbanyi ametoa kauli hiyo mkoani Singida wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa bodi hiyo kinachoendelea kufanyika mkoani humo. Amesisitiza kuwa PSPTB haitasita kuwafuta au kuwachukulia hatua wataalamu wote wanaokwenda kinyume na maadili ya taaluma ya ununuzi na ugavi, lengo likiwa ni kulinda rasilimali za umma na kuimarisha uwajibikaji katika sekta hiyo nchini kote.

Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *