#HABARI: Serikali, kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), inatarajia kuzindua Kituo cha Kupoza na Kusambaza Umeme cha Mtera mkoani Iringa pamoja na kusaini mikataba ya kihistoria ya shilingi trilioni 1.2 kwa ajili ya kusambaza umeme katika vitongoji 9,009 nchini kote.

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy, amebainisha hayo jijini Dodoma kuwa matukio hayo yatafanyika Januari 16 na 17, 2026, yakishuhudiwa na Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, ikiwa ni hatua kubwa ya kutekeleza maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwafikishia wananchi nishati bora.

Kituo cha Mtera, kilichogharimu shilingi bilioni 9.2 kwa ufadhili wa Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Sweden na Norway, kitafungua njia kwa mradi kabambe wa miaka mitatu utakaotekelezwa na wakandarasi 30, wakiwemo wazawa 21.
Mradi huu unatajwa kuwa miongoni mwa miradi mikubwa zaidi kuwahi kutekelezwa na REA kutokana na ukubwa wa bajeti yake na idadi ya vitongoji vitakavyofikiwa katika mikoa yote ya Tanzania Bara, hali itakayosaidia kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda na biashara vijijini.

Mhandisi Saidy amewahimiza wananchi kuchangamkia fursa mbalimbali zitakazojitokeza wakati wa utekelezaji, ikiwemo ajira na biashara ya kutoa huduma kwa wakandarasi, huku akiwasihi kutumia umeme huo kuboresha huduma za kijamii na kuzalisha mali. Amesema mradi huo utakapokamilika utaifungua nchi kiuchumi na kuleta mapinduzi ya kimaendeleo katika maeneo yaliyokuwa yakisubiri huduma hiyo kwa muda mrefu, jambo litakaloinua kiwango cha maisha ya Watanzania wengi.

Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *