#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Tabora limefanikiwa kuwatia mbaroni watu 15 wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali, ikiwemo wizi wa pikipiki na vifaa vya ujenzi wa mradi wa maji wa Ziwa Victoria.

Kati ya watuhumiwa hao, sita wanadaiwa kuhusika na mauaji ya kinyama dhidi ya waendesha pikipiki wawili, Hamisi Nchambi na Sigela Hamis Maulid, ambapo inasemekana waliwanyonga na kuwapora simu, fedha, na pikipiki kisha kutelekeza miili yao katika maeneo tofauti mkoani humo.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa miili yao ilikutwa katika mazingira yanayofanana, ikiwa imefungwa kamba mikononi na miguuni.

Mwili wa Sigela Maulid (23) ulipatikana Januari 6 katika msitu wa Matitumbi, huku wa Hamisi Nchambi, maarufu kama Ngosha, ukikutwa umetelekezwa kwenye makaburi ya Miemba, Kata ya Malolo.

Operesheni hiyo ya Jeshi la Polisi imekuja kufuatia mfululizo wa matukio ya uhalifu yaliyoleta taharuki kwa wakazi wa Manispaa ya Tabora.

‎Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *