#HABARI: Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy, amewaelekeza wasimamizi wa miradi mikoani kuimarisha ushirikiano na viongozi wa maeneo husika ili kurahisisha usambazaji wa umeme.
Maelekezo haya yametolewa jijini Dodoma mara baada ya kusainiwa kwa mikataba ya kihistoria ya kusambaza umeme katika vitongoji 9,009 nchi nzima, hatua inayolenga kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wananchi kwa haraka.
Mhandisi Saidy amesisitiza umuhimu wa wasimamizi hao kufanya kazi kwa karibu na wabunge, viongozi wa mikoa, wilaya, na wakandarasi, huku akisisitiza kuwa wananchi wana matumaini makubwa na REA.
Amewataka kuzingatia sheria na miongozo ya Serikali katika utekelezaji, akibainisha kuwa mawasiliano mazuri kuanzia ngazi ya kitongoji hadi mkoa yatasaidia kutatua changamoto mapema na kuhakikisha miradi inakamilika kwa ubora.
Aidha, wakandarasi wametakiwa kutoa taarifa za kila siku kwa uongozi wa maeneo wanayofanyia kazi na kupewa kipaumbele wananchi wa maeneo hayo katika kutoa fursa za ajira. Wasimamizi wamehimizwa pia kushirikiana na taasisi nyingine kama TARURA na TFS ili kuondoa vikwazo vinavyoweza kujitokeza wakati wa ujenzi wa miundombinu hiyo ya nishati vijijini.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.