Katika ujumbe wa pongezi aliotoa kwa mnasaba wa kazi kubwa iliyofanywa na taifa kubwa la Iran katika kuandaa mikusanyiko mikubwa ya tarehe 12 Januari, na siku ya kihistoria iliyobuniwa kwa masaba huo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, taifa la Iran limewadhihirishia maadui ujasiri na utambulisho wake.

Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika ujumbe wa kupongeza kwa kazi kubwa iliyofanywa na taifa shupavu la Iran katika kuandaa mikusanyiko mikubwa ya kisiasa tarehe 22 Dei, sawa na Januari 12 amesisitiza kuwa: Taifa la Iran limewadhihirishia maadui, ujasiri na utambulisho wake, na hilo ni onyo kwa wanasiasa wa Marekani kuwa waache hila za kuwategemea mamluki wasaliti.

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa taifa la Iran, unasema: ‘Leo mlifanya kazi kubwa na kubuni siku ya kihistoria. Mikusanyiko hii mikubwa na iliyojaa azma imebatilisha njama ya maadui wa kigeni, ambayo ilipangwa kutekelezwa na mikono ya mamluki wa ndani.’

Kiongozi Muadhamu amesisitiza katika ujumbe wake kwamba, taifa la Iran lina nguvu na uwezo, uelewa, linamfahamu adui na lipo uwanjani wakati wote.

Mikusanyiko ya mshikamano wa kitaifa dhidi ya ugaidi wa Kizayuni na Marekani ilifanyika kote nchini Jumatatu, Januari 12, ikiwemo Tehran. Watu wa matabaka tofauti walionyesha kuchukizwa kwao na vitendo vya ugaidi vya siku chache zilizopita kupitia maandamano na mikusanyiko waliyofanya katika mikoa tofauti nchini.

Maandamano ya Dei 22 hayakuwa maandamano ya kawaida ya mitaani tu; bali kama hatua pana ya kijamii na kisiasa, ilibeba ujumbe muhimu wa ndani na nje ya nchi. Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amelitaja tukio hilo kuwa “siku ya kihistoria” na “kazi kubwa ya taifa la Iran.” Uchambuzi kuhusu mahudhurio haya makubwa pia unaonyesha kuwa tukio hili lilikuwa la matabaka na jumbe kadhaa za kimsingi. 

Mahudhurio makubwa ya watu kote nchini yamekuwa dhihirisho halisi la mamlaka ya kijamii na utambulisho wa kitaifa. Mahudhurio haya yanathibitisha wazi kuwa taifa la Iran lina uwezo wa kuhamasisha na kudhihirisha umoja wake katika hali na mazingira magumu. Katika ujumbe wake, Kiongozi Muadhamu amesisitiza kuwa taifa la Iran lina “nguvu, uwezo, uelewa na ufahamu wa kutosha kumhusu adui.” Maelezo haya yanadhihirisha ukweli kwamba wananchi wameonyesha utambulisho wao halisi wa kujitegemea na azma ya pamoja mbele ya maadui zao.

Mahudhurio makubwa ya wananchi katika maandamano ya tarehe 22 Dei

Moja ya mihimili mikuu ya ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi lilikuwa onyo kwa wanasiasa wa Marekani. Mahudhurio haya makubwa ya wananchi yameonyesha kuwa siasa za chuki za Ikulu ya White House zenye misingi ya mashinikizo, vikwazo na operesheni za kisaikolojia dhidi ya Iran hazina tija.

Umuhimu mwingine wa ushiriki mkubwa wa watu katika maandamano hayo ya tarehe 12 Januari ni mshikamano wa kitaifa na kuwa macho mbele ya njama ambazo makundi ya kigaidi kwa uungaji mkono wa Marekani na Magharibi, yamekuwa yakijaribu kuzitekeleza. Uwepo huu mkubwa umeonyesha kuwa kutegemea magaidi kwa ajili  ya kuvuruga usalama ndani ya Iran ni kazi bure. Hii ni katika hali ambayo taifa la Iran liko macho mbele ya hadaa za kisiasa za Marekani na lina jibu madhubuti na lililoratibiwa kwa vitisho vya kigeni.

Maandamano ya Dei 22 pia limekuwa jibu la kivitendo kwa ugaidi wa hivi karibuni wa maadui. Watu wote nchini wameonyesha kuchukizwa kwao na ugaidi unaochochewa na maadui, kwa kuingia mitaani na kuonyesha kwamba usalama wa taifa ni mstari mwekundu wa jamii ya Iran. Uwepo huu mkubwa pia umeonyesha kuwa vitisho vya usalama haviwafanyi watu kurudi nyuma, bali vinaimarisha zaidi mshikamano wa kitaifa.

Maadui walitaka kutumia vibaya maandamano ya hivi karibuni kwa kuibua ghasia na operesheni za kigaidi, lakini uwepo wa watu ulitumia vizuri nafasi ya kijamii nchini na hivyo kusambaratisha njama hiyo ya maadui. Uwepo huu bila shaka umeimarisha uwiano wa kitaifa. Kupitia uwepo wao, bila shaka wamepunguza taathira za vita mseto vya adui katika kiwango cha kijamii.

Maandamano ya Dei 22 yanaweza kuchukuliwa kuwa tukio lenye pande kadhaa ambalo limekuwa onyo kubwa kwa wanasiasa wa Marekani ili waache kutekeleza njama na kuibua migogoro dhidi ya taifda shupavu la Iran. Uwepo huu kwa mara nyingine tena umeonyesha kuwa taifa la Iran lina nafasi kubwa katika kudumisha usalama, uthabiti na uhuru wa nchi katika nyakati ngumu.

Tukio hili limethibitisha kuwa taifa la Iran, kwa kuwa na maarifa, nguvu na uwepo kwa wakati, bado ndilo tegemeo muhimu zaidi kwa mfumo na kizuizi kikuu zaidi dhidi ya njama za kigeni, na kila inapobidi, huamua mkondo wa matukio kwa hatua yake ya pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *