Risasi za kiwango cha kijeshi zinazohusishwa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel zimepatikana katika uchunguzi wa kitabibu wa miili ya watoto waliouawa na magaidi wakati wa ghasia za hivi karibuni zilizochochewa na serikali za kigeni nchini Iran

Akizungumza na shirika la habari la TASS la Russia siku ya Jumatano, afisa wa usalama a Iran ambaye hakutaka jina lake litajwe aliashiria visa vya wasichana wawili waliouawa kwa risasi na mamluki wenye silaha katika miji ya Isfahan na Kermanshah. Kwa mujibu wa chanzo hicho, msichana wa aliyekuwa na miaka minane wa Isfahan alipigwa risasi tumboni, kwenye kidevu na nyuma ya kichwa wakati akiwa dukani na familia yake, na uchunguzi wa kitabibu wa mwili wake ulionyesha kuwa risasi za kijeshi zinazohusishwa na Israel ndizo zilizotumika katika shambulio hilo.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa tukio la pili linamhusu Melina Asadi, aliyekuwa na umri wa miaka mitatu, ambaye alipigwa risasi kutoka nyuma na magaidi mjini Kermanshah tarehe 7 Januari wakati akirejea nyumbani na baba yake kutoka duka la dawa.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, matatizo ya kiuchumi yaliyosababishwa na kuongezwa na miaka ya vikwazo vya Magharibi yalichochea wimbi la maandamano ya amani miongoni mwa wafanyabiashara katika mji mkuu wa Iran, Tehran, na miji mingine. Mamlaka zilitambua madai ya waandamanaji kuwa ya msingi, lakini maandamano hayo yalitekwa na wahuni walioungwa mkono na watawala wa Marekani na Israel, ambao walitoa wito wa wazi wa uharibifu na vurugu.

Maafisa walisema kuwa baadhi ya mamluki walikuwa wamejihami, wamefunzwa na kuajiriwa na mashirika ya kijasusi ya Marekani na Israel kwa lengo la kuchochea vurugu, kuharibu mali ya umma na kuua raia pamoja na maafisa wa usalama. Katika taarifa iliyotolewa Jumatano, Taasisi ya Mashahidi na Maveterani ya Iran ilisema jumla ya watu 3,117 walipoteza maisha wakati wa ghasia hizo. Iliongeza kuwa kati ya hao, 2,427 walikuwa raia wasio na hatia na maafisa wa usalama. Taarifa hiyo ilibainisha kuwa wengi wa mashahidi hao walikuwa wapita njia na waandamanaji waliouawa kwa risasi na vikundi vya kigaidi vilivyoandaliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *