Waasi wa M 23 wanaendelea kujiimarisha zaidi kisiasa na kiuchumi, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, licha ya kuwepo kwa mkataba wa kusitisha vita, ambao utekelezwaji wake, unaendelea kusuasua.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

M 23  wameendelea kuwaajiri wafanyakazi katika maeneo wanayodhibiti, jijini Goma na Bukuvu, na hata kukusanya ushuru. Aidha, wanatoa mafunzo kwa Majaji, polisi na wanajeshi, ili kuunda serikali yake kama ile ya Kinshasa.

Licha ya hatua hii, serikali ya Kinshasa, imefunga Benki na taasisi zake zote za fedha, pamoja na ofisi za serikali huku, watumishi wa umma wakikimbilia miji mingine.

Viongizi wa M 23, wakiongozwa na Corneille Nangaa, wanasema, lengo ni kumwondoa madarakani rais Felix Tshisekedi na kuunda serikali mpya, jijini Kinshasa.

Joseph Kabila - Rais wa zamani wa Congo ambaye anatuhumiwa na Kinshasa kwa kuwaunga mkono waasi wa M23.
Joseph Kabila – Rais wa zamani wa Congo ambaye anatuhumiwa na Kinshasa kwa kuwaunga mkono waasi wa M23. © JOSPIN MWISHA / AFP

Hivi karibuni, M 23 walitangaza kuwa, wamewaajiri na kuwapa mafunzo wanajeshi wapya zaidi ya 7,000, na kuzua maswali inakotoa fedha, na inaendeshaje shughuli zake bila kuwepo kwa Benki katika eneo hilo.

Wachambuzi wa mambo wanasema, mikakati ya M23 ni kuwaonesha wananchi na jumuiya ya Kimataifa kuwa, wana uwezo wa kuongoza nchi hiyo kubwa yenye rasilimali nyingi barani Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *