
Sébastien Lecornu ambaye amejiuzulu kwene wadhifa wa Waziri mkuu wa Ufaransa amesema kuwa masharti hayakuweza kutimiwza ili kuwa waziri mkuu. Hayo ni baada ya kujiuzu kwenye wadhifa huo Jumatatu, Oktoba 6.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Sébastien Lecornu ambaye aliteuliwa mnamo Septemba 9 kwenye wadhifa huo, alikosolewa na upinzani na mrengo wa kulia baada ya kutangaza sehemu ya serikali yake siku ya Jumapili, Oktoba 5. Alipaswa kuwasilisha taarifa yake ya jumla ya sera katika Bunge la taifa siku ya Jumanne.
Katibu wa Chama cha Kisoshalisti akaribisha kujiuzulu kwa Lecornu
Olivier Faure amekaribisha kujiuzulu “kwa heshima na taadhima” kwa Sébastien Lecornu, ambaye anamtaja kama “mwanasera wa Gaule.” “Nilikuwa nikijiuliza kama kweli kuna na kiongozi ambaye bado anasera za Gaule katika nchi hii. Alikuwa mmoja tu,” amesema katibu wa kwanza wa Chama cha Kisoshalisti kwenye mtandao wa kijamii wa X, kufuatia taarifa ya Sébastien Lecornu huko Matignon. “Amejiuzulu kwa heshima na taadhima,” amesema.
Kulingana na wachambuzi wa kisiasa, hatua hii inalitumbukiza zaidi taifa hilo la Ulaya kwenye mkwamo wa kisiasa.
Sébastien Lecornu alijutia matokeo haya yasiyotarajiwa, ikizingatiwa kwamba njia nyingi za mazungumzo zilikuwa zimechunguzwa. Amesema “amejaribu kujenga njia […] kuhusu masuala ambayo yalikuwa yamezuiliwa,” kama vile bima ya ukosefu wa ajira na usalama wa kijamii”.
Alijitetea kwa kueleza kuwa kila alipohisi anapiga hatua, mistari inarudi nyuma na madai yanaongezeka, ambapo kulingana na yeye, itachukua muda kufikia makubaliano ya bajeti. Pia amesikitishwa na “kuamka kwa baadhi ya tama za ushabiki” wakati wa muundo wa serikali, akieleza kuwa hiyo ni sababu mojawapo iliyomfanya ajiuzulu. “Lazima kila wakati upende nchi yako kuliko chama chako,” amesema kwa dokezo la wazi kwa rais wa LR, Bruno Retailleau, ambaye siku ya Jumapili jioni aliharakisha mchakato wa kujiuzulu kwake kwa kutilia shaka ushiriki wa Republican katika serikali mara tu itakapoundwa.