
Retailleau kutoka chama cha siasa za mrengo wa kulia cha Les Republicains (LR) ameongeza kuwa kuna hatua zingine zinazoweza kuchukuliwa kabla ya kufikia kwenye uchaguzi huku akisema kuwa yeye si mwenye maamuzi lakini akamtaka Rais Emmanuel Macron kulizungumzia suala hilo haraka iwezekanavyo.
Kauli hiyo imetolewa wakati Waziri Mkuu wa Ufaransa Sebastien Lecornu aliyechukua wadhifa huo mwezi uliopita kutangaza kujiuzulu leo katika hali ambayo haikutarajiwa, na ikiwa ni saa chache baada ya kuteua baraza lake jipya la mawaziri, ambapo nafasi nyingi muhimu zilionekana kuendelea kushikiliwa na mawaziri waliokuwepo, hatua iliyokosolewa vikali na upinzani uliotishia kuiangusha serikali yake.