Katika mazungumzo ya Misri yasiyo ya moja kwa moja kati ya Hamas na Israel, Mjumbe mkuu wa Hamas, Khalil El-Hayya, amesema kundi hilo ‘linataka dhamana kutoka kwa Rais wa Marekani Trumpna nchi zinazodhamini kuwa vita vitamalizika kabisa mara moja na daima baada ya makubaliano kuridhiwa. Katika mahojiano yake na kituo cha  Al Qahera amesema hawana imani na Israel hata kidogo. Akisema Israel haijawahi kutimiza ahadi zake katika suala la uvamizi katika historia. Ameongeza kwa kusema  wameshuhudia hilo mara mbili katika vita vita hivi vinavyoendelea. Kwa hiyo, wanahitaji dhamana ya kweli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *