#HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Bw. Nickson Simon, amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Pwani, kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutumia majiko ya kisasa yanayotumia nishati safi ya kupikia, hatua hiyo itasaidia kutunza mazingira na kulinda afya zao kwa kuwa majiko hayo ni salama, rahisi kutumia na yanapatikana kwa bei nafuu, hivyo ni muhimu kuyatumia ili kuendana na dhamira ya serikali ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini.

Ameyasema hayo Kibaha mkoani Pwani, mara baada ya kukabidhiwa jiko la kisasa linalotumia nishati safi na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *