Kundi la waandamanaji siku ya Jumanne, Oktoba 7 waliandamana katikati ya jiji la Nairobi kuunga mkono Israel na kuiombea amani jijini Jerusalem.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Waandamanaji hao walibeba mabango yenye ujumbe-Israel ni ya Mungu, omba amani kwa ajili ya Jerusalem, huku wakipeperusha bendera ya Kenya, Israel na Marekani.
Maandamano hayo yalifanyika wakati Israeli ikiadhimisha miaka miwili, baada ya Hamas kuvamia Israel na kusababisha vita vinavyoendelea kwa sasa kwenye ukanda wa Gaza.

Mashambulio ya Hamas yamesababisha vifo vya watu 1200 na kuwateka watu 251, huku Israel ikiwauwa watu 67,000 kwenye ukanda wa Gaza.
Maandamano kuunga mkono wa Wapalestina na kushinikiza kumalizika kwa vita kwenye ukanda wa Gaza, pia yalifanyika jijini Nairobi mwezi Septemba.